Siyo utani Yanga wamepoteza mechi (4) Kati ya (5) zilizopita…..ndani ya hizo mechi Yanga wameruhusu goli (8) huku wao wakifunga goli (3) tu.
Hii ni ıshara Tosha kikosi hakina balance nzuri ya kujilinda na kushambulia…..yes! Yanga hawafungi Magoli ya kutosha Pia safu Yao ya ulinzi inavuja sana
KUELEKEA DIRISHA DOGO YANGA WANAHITAJI WACHEZAJI HAWA WATATU MUHIMU
1. Mlinzi wa Kati (centre-back)
Msimu huu Yanga wamekuwa na majeruhi wengi kwenye eneo la ulinzi,leo atakosekana Bacca,kesho utasikia Job anaumwa,kesho kutwa utasikia Andambwile kalazwa…Yani ni matatizo chungu tele,mbaya zaidi hata wanaokuwa sawa viwango vyao vimeshuka sana mfano Bacca na Nondo siyo wale wa msimu jana.
Yanga wanatakiwa kupata beki mwingine wa Kati ambae atakuja kuleta ushindani na quality ya tofauti
2. Kiungo Mzuiaji (Pure Defensive midfielder)
Msimu huu Aucho ameshuka sana pia injury zinamsumbua sana,then Kati ya Duke na Mudathr,hakuna namba 6 wote ni Box to Box ambao wanaenjoy kwenda mbele kushambulia,hivyo Yanga wakishambuliwa ni rahisi Diarra kufikiwa……Yanga lazima watafute “defensive midfielder” haraka sana
3. Mbwa mwitu kwenye Box (Prolific number 9)
Yanga wanahitaji “A gun man” wanatakiwa kupata namba 9 wa maana hakara iwezekananyo…..Dube na Baleke bado hawaonyeshi mwanga….pia Musonda Siyo standing number 9 Muda mwingi anaenjoy kutokea pembeni.
Kama Yanga watafanikiwa kupata hao Wachezaji sahihi kwa wakati sahihi basi timu itarudi kwenye ubora wake
By Hans Rafael