Klabu ya Yanga SC imefanya mazungumzo na Kiungo Aziz Andabwile ili kufikia makubaliano ya kuachana nae katika dirisha dogo la uhamisho.
Kiungo Aziz Andabwile anatajwa kupisha usajili mpya wa Yanga SC katika maboresho ya klabu hiyo.
Aziz Andabwile aliwahi kucheza katika klabu ya Mbeya City FC kabla hajajiunga na Singida Big Stars.