YANGA WADAIWA SUGU TENA
Taarifa kutoka FIFA ni kwamba klabu ya Yanga imefungiwa kusajili mpaka itakapoilipa klabu ya Benchem United kiasi cha $ 80,000 (Sh 208milioni) kupitia usajili wa Augustin Okrah.
Awali huko nyuma Yanga ulifungiwa tena na FIFA kwa kushindwa kulipa stahiki za wachezaji watatu, Lazarous Kambole, Augustine Okrah na Afiz Konkon.