PRESHA KWA KOCHA MC ALGER MECHI SITA [6] ZA MWISHO IMESHINDA MOJA [1]
Ukitembelea Mitandao ya Kijamii ya Algeria utakutana na hisia za Mashabiki wa klabu ya MC Alger juu ya kutoka na Imani na Kocha wao Patrice Baumele.
Kocha huyu mfaransa aliwahi kuifundisha Ivory Coast Ingawa alishindwa kuipeleka FIFA Kombe la Dunia 2022 msimu Jana alifanikiwa kubeba ubingwa wa Algeria akiwa na Miamba hiyo ya Algiers.
Msimu huu licha ya kua nafasi ya pili kwenye msimamo nyuma ya CS Constantine bado kiwango chake kwenye michezo sita ya mwisho hakifurahishi.
TP Mazembe 0-0 MC Alger
Setif 0-0 Mc Alger
MC Alger 1-3 CR Belouizdad
El Bayadh 0-1 MC Alger
MC Alger 0-0 Biskra
MC Alger 0-0 Olympic Akbou
.
Matokeo haya yanapeleka Presha Kwa Kocha baadhi ya mashabiki wakitaka afutwe kazi kwani mambo yanamuendea kombo huku wakiwa na Matumaini makubwa ya kufanya vyema kimataifa.
.