Mechi imeisha, furaha ni kwa wanaYanga kushinda 4-0 na kiwango kikubwa kisicho na shaka ya aina yeyote. Yanga ilifanikiwa wapi?
Kwanza ni mabadiliko ya namna nzima Yanga ilivyokua inakaba ilipokua haina mpira (Out of possession). Alichonifurahisha Ramovic ni kuisuka Yanga kusaka mpira kwa kasi pale inapoupoteza na kuhakikisha unapatikana chini ya sekunde 45 za kazi. Anguko la Prison leo lilianzia hapa.
Pressing ya Yanga ilikua inahusisha wachezaji watatu mpaka wanne kwa wakati mmoja. Prison ilishinda kuhimili vishindo. Ushahidi wa hili linatokea wapi?
Goli la pili la Yanga lilitoka na Prison wakiwa na mpira kwenye eneo lao wakifanya build-up, Yanga ilifanya pressing kupitia Mzize, Farid Mussa na Mudathir. Prison ikapoteza mpira, Mzize akapiga pasi kwa Aziz Ki ambae alitoa ya pasi ya upendo kwa Dube, na mwana wa mfalme akaweka bao lake la 4 msimu huu.
Ramovic alizid kunifurahisha alipoamua kumuamini tena Kibwana Shomari leo hii katika nafasi ya beki wa kulia. Kibwana alikua ametulia kukaba na kushambulia. Huku nikiona mabadiliko zaidi ya role ya kibwana Yanga wakiwa na mpira. Alipewa maelekezo ya kuingia ndani kuongeza namba kwenye midfieled ( Inverting). Katika majukumu haya, Kibwana alicheza kwa akili na ubunifu mkubwa. Top perfomance.
Prison wamemaliza mechi hawana shot on target. Hili halikutokea kwa bahati mbaya, leo Yanga walikua na total dominance in and out of possesion. Nilipenda speed yao na maamuzi sahihi katika phase ya mchezo.
Mechi ya tatu mfululizo Dube anafunga. Mechi 3, bao 5. Confidence imerudi, overall game play yake ni ya viwango vya SGR. Leo akifunga na kutoa assist. Mwana wa mfalme akizidi kuonyesha thamani halisi ya kuhitajika ndani ya timu ya wananchi.
Man of the match kwa Bacca. Yes! Alistahili. Uwezo mkubwa, umakini na ufanisi. Bao moja alilofunga leo anafikisha jumla ya bao 3 kwenye ligi. Bao ambalo linahesabika la pili kwake kwenye mechi ya leo, marudio ya picha za Azam zinaonyesha mpira ulimgonga kipa kwenye kisogo. Tofauti na hapo, Bacca alistahili tuzo ya man of the match
Next match: Dec 29, Yanga vs Fountain Gate