Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz Yericko Nyerere @YerickoNyerereT ambaye katika mchakato wa ndani ya chama hicho wa uchaguzi unaoendelea ameweka wazi kuwa ni shauku yake kuona Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe @freemanmbowetz anastahili kuendelea kuiongoza CHADEMA kwa miaka mingine mitano mara zote amekuwa akitoa sababu lukuki za kuthibitisha kile anachokiamini kuhusu Mbowe
Kupitia machapisho yake tofauti tofauti ya mitandao ya kijamii Yericko Nyerere ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CHADEMA amekuwa akimshushia lawama na kumkosoa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara Tundu Lissu @TunduALissu ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti Taifa kwa kile anachodai kuwa hana sifa za kushika nafasi hiyo anayowania
"Nilipoeleza katika makala kuu (makala iliyoangazia kwa namna gani anamuamini Mbowe kuliko Lissu kwa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) kwamba Lissu hana sifa za kuwa Mwemyekiti wa CHADEMA Taifa kwa sababu ni muongo wengi mlipinga na matusi juu, niliorodhesha uongo wake mwingi ikiwemo uzushi wake juu ya kinachoitwa mabilioni ya Abdul, sasa akiwa Maria space alimtuhumu na kumzuishia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwamba alijiamulia yeye binafsi kumualika Mheshimuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan @SuluhuSamia kwenye kongamano la BAWACHA na kutoa tuzo" -Yericko
"Sasa ushahidi mwingine wa uongo wa Lissu ni katika video (ameambatanisha video kwenye chapisho lake) sauti akisikika akimsifu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na uamuzi wa chama kumwalika katika kongamano hilo, hii ikithibitisha kuwa Lissu alishiriki kumwalika Rais kwenye kongamano hilo, kwa namna Lissu alivyokidhalilisha chama huko nyuma na akikituhumu chama na viongozi wake kwa mambo mbalimbali, akitoa siri za Kamati Kuu na kukibagaza chama vilivyo nadiriki kusema Lissu anakosa sifa hata ya kuwa mwanachama tu wa CHADEMA, kama kamati ya uchaguzi itafuata kanuni za uchaguzi, basi Lissu anatakiwa kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hiki kwakuwa amevunja maadili na kanuni za uchaguzi" -Yericko
"Kamati Kuu ya chama ina kiapo cha wajumbe kuhakikisha wanalinda siri za chama na haitatokea mjumbe wa aina yoyote kutoa au kuzungumza mambo yaliyojadiliwa katika