Zitto Kabwe: Gari Lililomteka Nondo Tumelikuta Polisi Gogoni

Zitto Kabwe: Gari Lililomteka Nondo Tumelikuta Polisi Gogoni

Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema wamejulishwa kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa ACT, Abdul Nondo amefichwa kituo cha polisi Gogoni, Kibamba Dar es Salaam.

Zitto Kabwe amesema “Tumefika Kituoni, ingawa Polisi wamekataa, tumekuta Landcruiser iliyotumika kumteka Nondo ikiwa inabadilishwa number plates (kutoka zile za IST zilizotangazwa na Msemaji wa polisi na kuwekwa zingine), pichani ndio gari iliyomteka Nondo ikiwa Kituo cha Polisi Gogoni, Kibamba”

“Polisi ni dhahiri mpo na Nondo, tafadhali mwacheni huru akiwa mzima wa afya BILA HATA MCHUBUKO! Tafadhali Tafadhali Tafadhali!”

Itakumbukwa mapema leo Jeshi la Polisi lilisema leo December 01,2024 majira ya saa 11.00 alfajiri katika eneo la stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es salaam kuna Mtu mmoja Mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na Watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili wa namba T 249 CMV aina ya Landcruiser rangi nyeupe na kwamba ilielezwa na Mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baaadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa ni vya Abdul Omary Nondo “Ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza mara tu baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo Polisi, sambamba na kufungua jalada”

Millard

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad