Ahmed Ally Afunguka Simba Kutoka Sare na Bravos, Akitaka Namba Moja
Meneja wa habari na mawasiliano klabu ya Simba SC ametoa kauli yake baada ya Simba SC kupata pointi moja kwenye michuano yao dhidi ya Bravos ya Angola. Simba SC walisafiri siku ya Alhamisi alfajiri wiki iliyopita kuelekea nchini Angola kukutana na Bravos.
Ahmed Ally amesema kuwa kazi ya kwanza ya kutinga robo fainali ilikamilika jana. Ametoa utabiri wake kuwa timu ya Simba SC itafuzu hadi robo fainali. Jambo ambalo limezua mijadala mbalimbali mitandaoni hasa kwa mashabiki wengi wa Simba.
Constantine wapo kwenye nafasi ya kwanza kwenye Msimamo wa Kombe la Shirikisho Afrika kundi la A. Wapo na pointi kumi na mbili. Simba SC wapo kwenye nafasi ya pili wakiwa na alama kumi. Iwapo Simba watashinda mchezo wao wa nyumbani dhidi ya MC Alger watapanda hadi nafasi ya kwanza kwenye Msimamo huo. Watafisha pointi kumi na tatu.
"Kazi ya kwanza kutinga robo fainali imefanikiwa,bado kazi ya pili kuongoza kwenye msimamo wa Kombe la Shirikisho Afrika kundi la A," Ahmed Ally amesema baada ya Simba SC kuenda sare.