Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amemtaka kocha mkuu wa klabu ya Yanga kuomba radhi baada ya kuiita Ligi ya Tanzania Bara dhaifu.
“Kocha Ramovic anapaswa kuomba radhi kwa kuiita Ligi ya Tanzania dhaifu, au afukuzwe. Kama ligi yetu ni dhaifu mbona amekuja kufundisha huku? Hii kauli inapaswa kupingwa vikali."
- Ahmed Ally, Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba.