Ajali ya Ndege Kenya, Yaangukia Waendesha Boda Boda na Kuua



Watu watatu wamefariki baada ya Ndege aina ya Cessna 172 inayomilikiwa na Chuo cha Aeronautical cha Nchini Kenya kuanguka na kuwaka moto eneo la Kwa Chocha, Malindi.

Waliofariki ni pamoja na waendesha bodaboda wawili na abiria, huku mwendesha pikipiki mmoja akiteketea kiasi cha kutotambulika wakati akijaribu kuokoa pikipiki yake.


Nahodha, mkufunzi na Mwalimu wa ndege hiyo wao walinusurika katika ajali hiyo na kupelekwa katika hospitali ya Tawfiq wakiwa katika hali nzuri.

Mamlaka za kiusalama za Kenya zilithibitisha tukio hilo na kudai kuwa uchunguzi wa ajali hiyo iliyosababisha uharibifu mkubwa kwa majengo ya karibu unaendelea.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad