Meneja wa habari na mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amevunja ukimya wake baada ya Yanga SC Kuifumua Al Hilal ya Sudan. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, Young Africans waliweza kufunga bao moja dhidi ya Al Hilal siku ya Jumapili Januari 12,2025. Hii ni hatua muhimu kwa wananchi. Hadi sasa Young Africans wapo kwenye nafasi ya tatu wakiwa na alama saba. Iwapo watashinda mchezo wao wa tarehe 18, watachukua nafasi ya pili na alama kumi. Hadi sasa vinara wa kundi hilo Al Hilal wapo na pointi kumi.
"Waarabu watakwenda kuitapika hiyo pointi moja dimbani Benjamin Mkapa". Maneno ya Ally Kamwe akizungumzia mchezo wao wa tarehe 18, 2025 ndani ya dimba la Benjamin Mkapa dhidi ya MC Alger.
Ni mchezo wa mwisho kwa timu zote mbili katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) huku akiwaita mashabiki kubeba vichinjio vyao. Yanga SC jana Jumapili ilishinda kwa goli dhidi ya Al Hilal ya Sudan na kufikisha pointi saba huku MC Alger wapo na pointi nane.