Aliyefanya Upasuaji ili Afanane na Paka Afariki Dunia
Jocelyn Wildenstein Mwanamke aliyejipatia umaarufu kwa sura yake ya kipekee baada ya kufanyiwa upasuaji ili kufanana na Paka amefariki dunia akiwa na miaka 84 huko Jijini Paris kutokana na matatizo ya mapafu kwa mujibu wa Mchumba wake Lloyd Klein.
Jocelyn alitumia mamilioni ya pesa kubadili sura yake akivutiwa na macho ya Paka na mashavu yalioinuka ambapo muonekano wake huo ulimpa jina la Catwoman.
Mbali na muonekano wake, Jocelyn alijulikana kwa maisha ya kifahari na tukio la talaka yake ya kihistoria kutoka kwa Bilionea Alec Wildenstein ambapo alipokea mabilioni ya dola baada ya kuachana na Bilionea huyo.
Kifo chake kimeibua hisia mitandaoni ambapo Mashabiki zake wakimkumbuka kama Mtu aliyekuwa na ujasiri wa kuishi maisha ya kipekee na ya tofauti.