Aliyewaokoa Watumishi wa TRA Tegeta Apewa Tuzo...



Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkabidhi tuzo na zawadi ya Tsh. milioni 5, Mkazi wa Tegeta Jijini Dar es salaaam, John Malole ambaye aliwaokoa Watumishi wa TRA walioshambuliwa Tegeta Jijini Dar es salaam wakati wakitimiza wajibu wao baada ya kuhisiwa kuwa ni Watekaji.

Rais amekabidhi tuzo hiyo katika usiku wa tuzo za walipa kodi 2023/2024 unaoendelea usiku wa leo January 23,2025 Masaki Jijini Dar es salaam.

John aliwaokoa na kuwapeleka Hospitali Amani Simbayao na Watumishi wenzake wawili wa TRA walioshambuliwa wakati wakilifuatilia gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ambalo imedaiwa liliingizwa Nchini kinyemela bila kulipa kodi stahiki za Serikali ambapo wakati wakiwa kwenye pilikapilika hizo walihisiwa kuwa ni Watekaji na kuanza kushambuliwa, ambapo baadaye Amani alifia Hospitali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad