Mwanaume mmoja aitwaye Anwar ul-Haq, aliyekuwa ameirejesha familia yake Pakistan baada ya kuishi Marekani kwa miaka 25, amekiri kumuua binti yake wa miaka 15 kwa kumpiga risasi kutokana na kutoridhishwa na maudhui aliyokuwa akichapisha kwenye mtandao wa TikTok.
Mauaji hayo yalitokea Jumanne katika mji wa Quetta, Kusini magharibi mwa nchi hiyo, ambapo polisi wamesema mshukiwa awali alidai kuwa watu wasiojulikana walimpiga risasi binti yake mzaliwa wa Marekani kabla ya kukiri kuwa yeye ndiye aliyefanya kitendo hicho.
"Uchunguzi wetu hadi sasa umebaini kuwa familia ilikuwa na pingamizi kuhusu mavazi yake, mtindo wa maisha, na mikusanyiko yake ya kijamii," amesema mpelelezi wa polisi, Zohaib Mohsin.