Baada ya miezi kadhaa ya tetesi kuhusu hali ya ndoa maarufu zaidi katika siasa, Barack Obama alichapisha ujumbe wa upendo kwa mkewe, Michelle Obama, kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya miaka 61 ya mkewe Ijumaa. Alimwandikia: “Unajaza kila chumba kwa joto, hekima, ucheshi, na neema – na unavyojivunia kufanya hivyo. Nimebahatika kuwa na wewe katika kila changamoto ya maisha. Nakupenda!” Alijibu mkewe Michelle kwa kusema, "Nakupenda, mpenzi!"
Ujumbe huu wa upendo aliuandika huku tetesi zikizidi kusambaa kwamba ndoa yao ilikuwa kwenye matatizo. Hali ilianza kuchocheka baada ya Michelle kutokuwepo kwenye mazishi ya Rais mstaafu Jimmy Carter Januari 9, na kuongezeka zaidi baada ya kutangazwa kuwa hatahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Donald Trump leo.
“Michelle hawezi kuamrishwa na mtu yeyote – hakuna anayemwambia afanye nini,” alisema chanzo kilichofanya kazi na familia ya Obama. “Hiyo ndiyo sababu alishindwa kushawishika kumuunga mkono Joe Biden kwenye uchaguzi uliopita.” Aliongeza kusema kuwa Michelle hakuwepo kwenye mazishi ya Carter kwa kuwa alikuwa Hawaii kwa likizo ndefu.
Hata hivyo, baadhi ya watu wa karibu wanasema kuwa Michelle amekuwa mbali na maisha ya kisiasa tangu walipoondoka White House Januari 2017, jambo linalochochea uvumi kuhusu kutoridhika na mume wake na siasa kwa jumla.