Bob Wangwe Afunguka "Lissu Ataleta Mageuzi Ndani ya Chadema"

Bob Wangwe Afunguka "Lissu Ataleta Mageuzi Ndani ya Chadema"

Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @chadematzofficial Bob Chacha Wangwe @BobWangwe amesema ameamua kuweka wazi msimamo wake wa kwamba anamuunga mkono Tundu Lissu @TunduALissu badala ya Freeman Mbowe @freemanmbowetz katika mchakato wa kinyang'anyiro cha kumtafuta Mwenyekiti wa chama hicho Taifa kutokana na mahitaji ya sasa ya kisiasa yaliyopo hapa nchini ambayo anaamini mtu sahihi wa kuikomboa CHADEMA ni Lissu


Akihojiwa na Jambo TV leo, Ijumaa Januari 03.2024 Bob amesema katika nyakati hizi ambazo mazingira ya siasa na demokrasia ya Tanzania imeminywa kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua ya kile alichodai uporaji wa chaguzi mbalimbali za Kitaifa, uwepo wa matukio ya utekaji na mauaji hasa kwa wafuasi wa chama hicho, uwepo wa tuhuma za rushwa miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama hicho nk, ni wazi kuwa CHADEMA inahitaji mtu anayeweza kusimama kidete dhidi ya nguvu ya watawala (CCM na serikali yake) na kuhakikisha anaongoza harakati za mageuzi ya kweli


Amesema licha ya kwamba anatambua kazi kubwa iliyofanywa na Freeman Mbowe katika kipindi chote cha takribani miaka 21 aliyoongoza chama hicho kama Mwenyekiti wa Taifa, lakini yeye mwenyewe (Mbowe) ni vyema angetumia busara zake kutochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo tena ili kutoa nafasi kwa Tundu Lissu ambaye kwa mujibu wa Bob anaamini kwamba ni turufu nzuri kwa chama hicho kuelekea kwenye mageuzi wanayoyapigia kelele kwa muda mrefu


Kuhusu madai yanayoeleza kuwa endapo Lissu atachaguliwa kuongoza chama hicho basi hakitakuwa salama kutokana na misimamo yake ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kuathiri taasisi kwa kuwa hana busara, Bob anasema madai hayo sio ya msingi na kwamba ni vyema yakipuuzwa kwa kuwa hata sasa chama hicho hakiko salama


"Mpaka sasa hivi chama hakiko salama, kwa maana ya usalama ambao tunauzungumzia nathubutu kusema chama hakiko salama, ndio maana hadi sasa unaona watu wanakamatwa, wanatekwa, wanauawa, na mbaya zaidi tunaelezwa kwamba sasa hivi kuna harufu hadi za rushwa kwa baadhi ya viongozi, lakini pia kumekuwa na shida kwenye sekretarieti ya chama kwamba taarifa za siri zinavuja sana"....

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad