Mkongwe wa Ndondi, #MikeTyson ambaye ana umri wa Miaka 58 anapanga kurejea ulingoni kupigana baada ya kupoteza pambano dhidi ya Jake Paul (28), Novemba 15, 2024 ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kustaafu Miaka 20 iliyopita
Inadaiwa mpango uliopo ni Tyson kupigana na Mkongwe mwenzake, Evander Holyfield (62) ambaye alipigana naye mara ya mwisho Mwaka 1996 kisha pambano likamalizika Raundi ya 11 baada ya Tyson kumng’ata sikio Evander
Holyfield naye alijaribu kurejea ulingoni Mwaka 2021 kwa kupigana na Mwanamichezo wa Mapigano ya MMA, Vitor Belfort (47). Holyfield alikubali kichapo katika Raundi ya Kwanza kwenye pambano hilo