Breaking News:
Kutoka ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam Wakili Deogratias Mahinyila @deogratiusmahinyila ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa @bavicha_taifa akimshinda Masoud Mambo @MASOUDMAMBO24 aliyekuwa anapambananae kwenye nafasi hiyo
Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa zilikuwa 317 huku moja (1) ikiharibika, katika kura hizo Wakili Deogratias Mahinyila amepata kura 204 sawa na asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa huku Masoud Mambo aakipata kura 112 asilimia 35.3 ya kura zote zilizopigwa