"Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la uongozi wa chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu." - Freeman Mbowe
Tundu Lissu amuondoa Mbowe Uwenyekiti Chadema baada ya Utawala wa miaka 20
Tundu Lissu ameshinda kwa kishindo nafasi ya Uwenyekiti wa Chadema dhidi ya mpinzani wake mkubwa Freeman Mbowe ambaye amehudumu nafasi hiyo kwa miaka zaidi ya ishirini.
Wawili hao walichuana vikali katika kinyang’anyiro hicho kila mmoja akionyesha umwamba wake hali ambayo ilisababisha uchaguzi kuwa na msisimko mkubwa.