CAF Yaongeza Fedha Kwa Mshindi wa Kombe la CHAN

CAF Yaongeza Fedha Kwa Mshindi wa Kombe la CHAN

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza ongezeko la asilimia 75 kwa atakayebeba Kombe la CHAN ambapo mshindi sasa atapata Dola za Kimarekani Milioni 3.5.

CAF pia ilitangaza kuwa jumla ya pesa za tuzo za CHAN Kenya, Tanzania na Uganda 2024 zimeongezwa hadi Dola Milioni 10.4 ikiwa ni ongezeko la 32%.

CHAN ni Mashindano muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa wachezaji wa soka barani Afrika na wachezaji chipukizi wenye vipaji na yatachangia pakubwa katika ushindani wa kimataifa wa soka la Afrika na Mashindano ya CAF.

Mashindano haya ni sehemu ya mkakati wa kuwekeza katika soka la Afrika na kuifanya kuvutia mashabiki wa soka, watazamaji, wadhamini, washirika na wadau wengine barani Afrika na duniani kote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad