Chama Kucheza na Kifaa Maalumu Mkononi....



DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Yanga, Clatous Chama amerejea mazoezini na anatarajiwa kufungwa kifaa maalum mkononi ili kuikabili TP Mazembe, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nyota wengine wawili Djigui Diarra, Max Nzengeli wamerejea uwanjani wakiwa tayari kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi.

Nyota hao wamekosekana katika baadhi ya michezo kutokana na majeraha ambayo yalikuwa yakiwakabili lakini sasa wamepona na wako tayari kuitetea nembo ya Yanga.

Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe alithibitisha kwa kusema kuwa, baada ya kukaa nje kwa michezo kadhaa, wachezaji hao watatu wamerejea uwanjani kufanya mazoezi ya ushindani huku Chama akitarajiwa kufungwa kifaa maalum mkononi.

“Diara, Max wapo fiti kuelekea mchezo wa Jumamosi, Chama naye yupo kwenye mipango lakini daktari ameshauri kama atacheza basi atalazimika kufungwa kifaa maalum mkononi kumsaidia na purukushani za mchezo dhidi ya TP Mazembe,” amesema.

Amesema vipimo vya madaktari wa timu hiyo vimejiridhisha kuwa, mastaa hao wapo kamili na tayari wanaendelea na mazoezi wakiwa kwenye mipango ya kocha Sead Ramovic kuelekea mechi hiyo.

“Hali ya wachezaji hao ipo vizuri, isipokuwa Aziz Andambwile bado hajakuwa fiti. Tunaamini kuwa, watakuwa sehemu ya kikosi kitakachowavaa TP Mazembe mechi yetu ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambayo ni muhimu kushinda,” amesema.

Katika michuano hiyo, Yanga wako kundi A linaloongozwa na Al Hilal ya Sudan wenye alama tisa, MC Alger wenye alama nne nafasi ya pili, TP Mazembe nafasi ya tatu wakiwa na pointi mbili huku Yanga akiwa mwisho na alama moja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad