Chasambi wa Simba Alikoroga, Amtaja Mchezaji wa Yanga Max Nzengeli Kuwa Role Mode Wake

Chasambi wa Simba Alikoroga, Amtaja Mchezaji wa Yanga Max Nzengeli Kuwa Role Mode Wake

Chasambi wa Simba Alikoroga, Amtaja Mchezaji wa Yanga Max Nzengeli Kuwa Role Mode Wake

Kauli yenye utata? Ndio haitazama vema katika akili za mashabiki wa Simba. Nadhani mashabiki wa Simba watamuona mamluki. Baadaye hata viongozi wa Simba wanaweza kumhoji na kumlazimisha awaombe msamaha wachezaji wenzake.

Chasambi alisikika akisema kwamba hakuna mchezaji anayemtazama kama kioo chake (role modl) katika kikosi cha Simba. Alikwenda mbali zaidi na kutibua mambo kwa kudai kwamba katika ligi yetu mchezaji ambaye anamtazama kama kioo chake ni staa wa Yanga, Maxi Nzengeli. Hapo alikuwa ameharibu zaidi kwa mashabiki wa Simba kwa sababu amemtaja mchezaji kutoka kwa mahasimu wao Yanga.

Ukichunguza kauli ya Chasambi unaweza kumuelewa. Kama Chasambi angekuwa mchezaji anayecheza nafasi ya ulinzi ungeweza kumshangaa kidogo. Kwa mfano angekuwa anacheza kama beki wa kulia ungemshangaa. Kwanini kioo chake asiwe Shomari Kapombe? Kama angekuwa anacheza nafasi ya beki ya kushoto tungemuuliza kama anamuona Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ni mchezaji kawaida.

Tatizo ni kule mbele. Naamini kule mbele ambako Chasambi anacheza ndipo ambapo angeweza kumpata mchezaji kioo kwake. Na nadhani hata yeye alikuwa anazungumzia wachezaji wanaocheza mbele. Nadhani ndio maana alimtaja Maxi wa Yanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad