Bosi mmoja wa juu wa Yanga SC ameliambia Mwanaspoti kuwa, ukiacha ofa za klabu za Afrika Kaska-zini zilizofikia Sh2 Bilioni ambayo klabu yao ilipanga kumuuza sasa klabu hiyo ya Ubelgiji inataka kutoa zaidi ya fedha hizo kufikia 2.5 bilioni. Dau hilo limewachanganya mabosi wa Yanga SC na sasa wanafikiria kufanya biashara haraka kumpa fursa mshambuliaji huyo ambaye tayari msimu huu ameshafunga mabao sita kwenye Ligi Kuu pekee.
“Hii wikiendi ni vile tu hajacheza na hajafunga lakini akifunga tu utaona kuna barua pepe itaingia klabu zinauliza vipi jamani bado hamjafikiria,” alisema bosi huyo.
“Tunafikiria kufanya biashara fedha zinazosemwa ni nyingi unajua pia tunataka kufikiria juu ya maisha ya baadaye ya mchezaji ili akajiendeleze tutaangalia ofa ipi itakuwa sahihi zaidi kwa klabu na kwake.