Dkt. Philip Mpango Aomba Kujiuzulu Umakamo wa Raisi



Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemwandikia barua ya kuomba apumzike Umakamu wa Rais ambapo amesema baada ya kutafakari ameridhia ombi hilo lakini kwa sasa Dkt. Mpango ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.

Akiongea leo January 19,2025 kwenye Mkutano Mkuu Maalum Jijini Dodoma, Rais Samia amesema “Dkt. Philip Mpango ndiye Makamu wa Rais miezi ya karibuni hapa amekuja kuniona kuniomba apumzike, ana sababu kadhaa lakini sio za kazi, anasema yeye sasa ana miaka 68 na angependa kuishi zaidi kwahiyo naomba nipumzisheni, nikambishia bishia Wiki iliyopita hapa akanikabidhi barua yangu hii ( ya kujiuzulu) na barua sikumjibu, nilipoenda kwenye Kamati Kuu nikawaeleza hiyo hali na kwa pamoja wote tukakubali tumpumzishe”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad