Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (@chadematzofficial) na pia Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Willbroad Peter Slaa, amekamatwa na polisi usiku wa leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam huku sababu za kukamatwa kwake bado hazijawekwa wazi.
Akizungumza kwa njia ya simu Dkt. Slaa ameeleza kuwa, polisi wamefika nyumbani kwake na kumchukua na kuelekea naye kituo cha polisi Mbweni.
Taarifa zaidi zitawajia