Edo Kumwembe Afunguka Sababu za Chasambi Kumchagua Max Nzengele Kama Role Mode Wake

Edo Kumwembe Afunguka Sababu za Chasambi Kumchagua Max Nzengele Kama Role Mode Wake


Kwanini amemchagua Maxi? Nadhani jibu lake wengi tunalo. Kwake yeye mwenyewe Chasambi sijui kama atakuwa na jibu kama letu. Pale Yanga kuna wachezaji wengi wazuri na wenye majina makubwa katika eneo la mbele.

.

Wapo kina Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki, Prince Dube, Clement Mzize na wengineo. Hata hivyo zipo nyakati ambazo kila mchezaji anapokuwa chini basi Maxi anasimama na kuhesabiwa. Maxi anajaribu kufanya kila kitu uwanjani ikiwemo kumsaidia kocha katika kumchezesha nafasi tofauti ili mradi timu isonge mbele.

.

Maxi anajua kukaba, anajua kupandisha timu mbele, anajua kufunga. Sijui kama Chasambi amechagua jambo gani kati ya hayo, lakini hayo matatu ndio ambao yanamtofautisha Maxi na mastaa wengine wa Yanga. Kwa kocha ambaye anaabudu mpira wa kisasa, lazima Maxi awe chaguo lake namba moja mbele ya Aziz na Pacome kwa namna anavyofanya majukumu mengine uwanjani.

.

Sijui Chasambi amechagua kitu gani zaidi kwa Maxi, lakini sasa ni wakati wa kumpa changamoto yeye mwenyewe. Kama anaamini hakuna mchezaji kioo kwake pale Simba basi yeye mwenyewe awe kioo kwa wachezaji wengine pindi wanapoitazama Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad