Kocha, Saed Ramovic anaonekana kuanza kuijua timu yake. Hata ‘sub’ yake ya kwanza dhidi ya Al Hilal alikuja kuifanya dakika ya 87 wakati Aziz Ki alipompisha Kennedy Musonda. Inaonekana pia anajua namna gani ya kuwatumia washambuliaji wawili, Clement Mzize na Prince Dube kwa wakati mmoja.
.
Lakini sasa wana mechi ya machozi, jasho na damu dhidi ya MC Alger katika Uwanja wa Mkapa pale Temeke. Waliwahi kucheza mechi ya namna hii wakati walipotakiwa kuichapa CR Belouzidad mabao manne na kwenda hatua ya robo fainali na kweli walifanya hivyo. Joseph Guede aliziona nyavu za Belouzidad katika dakika za jioni.
.
Na sasa ni zamu ya kina Dube kufanya hivyo katika pambano hili la machozi, jasho na damu dhidi ya MC Alger ambao wanafahamu kuwa wanakuja vitani. Wakati mwingine Yanga na Simba zimezoea kujiweka katika mazingira magumu kisha zinajinasua. Yanga wana kazi chafu mkononi mwao Jumamosi ijayo.
.
KWANZA wanatakiwa WAJAE uwanjani kuipa mazingira magumu MC Alger. PILI wanatakiwa wapambane hasa kujaribu kupata bao au mabao ya MAPEMA. Waarabu watajaribu kucheza kwa akili kubwa ya kujihami mpaka pale watakapotanguliwa ndipo watagundua kwamba matokeo ya kufungwa hayasaidii. Wataondoka langoni mwao.
.
Vinginevyo watapoteza muda kadri watakavyoweza. Watajaribu kujihami kwa usahihi kadri watakavyoweza. Kisoka, narudia kwamba katika kundi hili hakukuwa na timu ya kupambana na Yanga kabla ya Yanga kupoteza fomu yake chini ya Gamondi. Ni Yanga wenyewe wamejitakia kuwa katika mazingira haya. Tukutane Lupaso Jumamosi.” — Legend Edo Kumwembe.