Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Kanda ya Kaskazini Godbless Lema @godblessjlema1 amesema anaamini kwenye uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama hicho (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) Tundu Lissu @tunduantiphaslissu anashinda na kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa huku John Heche @hechejohn akishinda na kuwa Makamu Mwenyekiti Bara.
Lema amesema baada ya watu hao kushinda ataungana nao ili kuisaidia CHADEMA kukua kiuchumi na kuleta mabadiliko hasa katika sekta ya fedha kwenye chama hicho.