Godbless Lema "Wenje Hastahili Kuwa CHADEMA ni Muongo Muongo"

Godbless Lema "Wenje Hastahili Kuwa CHADEMA ni Muongo Muongo"


 “Jana nilipoamka niliona tweet ya Mnyika na jana Waandishi mlikuwa na Wenje na nilimsikia, niliona alichokipata kule mitandaoni na Wananchi wote wa Tanzania, Wafuasi na Wadau mbalimbali wa sera za mabadiliko walivyotoa nidhamu na 70% ya Watu niliposema nitakuwa na press conference waliniambia nisimjibu kashajibiwa na Watanzania wamempa dozi maana unajua sasa hivi mitandaoni kuna uelewa mkubwa sana kwa Watu”


“Hata Mke wangu aliniambia nimsijibu na nilihisi kwasababu Wake zetu ni Marafiki lakini baadaye hata yeye alisema mtandaoni Watu wamemshughulikia usimjibu, nikasema lazima nimjibu baadaye nilipoona tweet ya Mh.Mnyika nikasema sidhani kama nitamjibu Wenje, na nilimpigia Katibu Mkuu leo alfajiri, nilipoisoma tena ila tweet niliongea na Mnyika ambaye ni Mtu mwenye utulivu sana lakini anafanya kazi kwenye mazingira magumu sana, niliona Watu wanamtukana Mnyika mtandaoni nikarudia kuisoma tena maana Mimi ni Mtu ninayefikiri sana”


“Ukiisoma tweet ya Mnyika ni nzuri ila hainiondoi Mimi kwenye uchafu na uongo uliosemwa na Wenje, Mimi ningefurahi kama Mnyika angesema ‘Wenje ni Muongo na join the chain ipo hivi …’ kisha akaendelea, imagine Wenje anataka kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa maana yake Mwenyekiti asipokuwepo huyo ndiye Mwenyekiti wenu, taswira ya Mtu muongo muongo hivi, anayebebwa bebwa na Wanaume wengine mara abebwe na akina Hussein, akina Abdul, ndio maana nilisema hastahili kuwa kwenye Chama hiki kama Chama hiki kinaamini katika values, hata mkishika madaraka na Chama cha upinzani kama mindset za hao Watu hazijawa transformed matokeo mtakayopata yanaweza kuwa mabaya kuliko mnayopata sasa kwa Chama tawala”


“Mfano kama msingi wa Chama unajengwa katika rushwa, hawa Watu hawapo kwenye power, na sisi lazima tushinde na Mh. Lissu tunashinda, maana yake tukishinda Kamati Kuu ya CHADEMA itakuwa inasimamia Serikali, mfano una Watu waongo na wala rushwa, wakiwa Ma-DC, Makatibu Wakuu n.k kwasababu msingi wa wao kupatikana hakuwa thabiti maana yake mtakuwa na hali mbaya, ndio maana Wana CHADEMA wanatakiwa kulinda values kwa uchungu mkubwa sana” ——— Godbless Lema akiongea Jijini Dar es salaam leo January 17,2025

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad