MKATABA wa golikiwa wa Yanga, Aboutwaleeb Mshery unatamatika mwisho wa msimu huu, lakini nyota huyo anadaiwa kuwagomea mabosi wake kuongeza mpya ikidaiwa kwamba anataka kujaribu changamoto sehemu nyingine.
.
Lakini, katikati ya ishu hiyo AZAM FC imeonyesha nia ya kumhitaji. Mshery ambaye hana namba katika kikosi cha kwanza chini ya Kocha Sead Ramovic ameomba kuondoka mwishoni mwa msimu huu.