Haji Manara Ampigia Debe Mbowe Uenyekiti wa Chadema....
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) @ccmtanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV, Haji Manara @hajismanara , ameonesha hisia zake kwa Mwenyekiti wa CHADEMA @chadematzofficial , Freeman Mbowe @freemanmbowetz , akieleza kuwa anatamani kuona Mbowe akiendelea kushika nafasi hiyo licha ya changamoto za kisiasa zinazokikumba chama hicho kuelekea uchaguzi wake wa ndani.
Manara, akizungumza kupitia mahojiano ya hivi karibuni ya Manara TV, ameeleza kuwa alitumia muda mrefu kutazama hotuba na majibu ya Mbowe kwenye mahojiano, huku akivutiwa na namna alivyoonesha busara na ukomavu wa kisiasa.
"Juzi nilikaa YouTube kwa saa mbili nikimwangalia Mbowe. Hotuba yake na namna alivyokuwa anajibu maswali, hata pale alipo-provokewa, ilinivutia sana. Mimi ukiniuliza, uchaguzi ukifanyika pale, ningetamani kuona Mbowe anaendelea kuwa Mwenyekiti," amesema Manara.
Pamoja na kumpongeza Tundu Lissu kwa kuwa mwanasiasa mzuri, Manara ameweka wazi kuwa Freeman Mbowe ni mmoja wa wanasiasa bora zaidi nchini Tanzania, akisisitiza kuwa busara zake ni muhimu kwa ustawi wa chama hicho na upinzani kwa ujumla.
Manara alisisitiza umuhimu wa upinzani thabiti kwa maendeleo ya taifa, akieleza kuwa chama chake cha CCM hakihitaji matusi bali changamoto zenye kujenga.
"Sisi CCM wa kisasa tunahitaji upinzani imara ili utukosoe, utupatie changamoto, na kuhakikisha miradi inatekelezwa. Hatuhitaji mtu aje na matusi. Tunataka upinzani imara ili viongozi wa serikali wasilale na kero za wananchi zitatuliwe," ameeleza Manara.
Manara ameongeza kwa kusema kuwa anatarajia upinzani kuwa thabiti na hatimaye kufikia hatua ya kuimarika kiasi cha kuchukua nafasi ya kuongoza kwa ‘kipindi kifupi’ kabla ya CCM kurejea madarakani.
"Baada ya kama miaka 50 au 100 ijayo, upinzani ukiimarika, basi tunaweza kuwaambia wachukue walau miaka mitano, kisha waturudishie utawala wetu," amesema kwa utani.