Haji Manara "Nimaumivu Makali Yanga Kupoteza Nafasi ya Robo Fainali



Haji Sunday Manara amevunja ukimya wake baada ya mechi ya jana. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, mechi ya MC Alger dhidi ya Young Africans ilimalizika sare ya sufuli. Ripoti imedai kuwa Yanga imeshindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa mara ya pili mfululizo baada ya jioni hii kumlazimisha sare na klabu ya MC Alger ya Algeria kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Timu hiyo inayonolewa na Mjerumani, Sead Ramovic ilihitaji kupata ushindi kwenye michuano hiyo ya aina yoyote ile ili kufuzu katika robo fainali kama ilivyofanya msimu uliopita ilipokuwa chini ya Kocha Miguel Gamondi aliyetimuliwa mara alipoiwezesha timu hiyo kutinga makundi ya michuano ya msimu huu.

Young Africans iliyokuwa na pointi saba ilihitaji ushindi ili kufikisha pointi ambazo zingewafanya kuungana na Al Hilal ya Sudan kwenda robo fainali. Licha ya Al Hilal kupokea kichapo kikali kutoka kwa TP Mazembe iliweza kuongoza kundi lao.

Haji Manara amedai kuwa, ni maumivu makali kwa wachezaji wa klabu ya Yanga baada ya kupoteza mechi ya jana.

"Ni maumivu makali kwenu wanaume. Naelewa namna mlivyoumia" Haji Manara ameandika katika ukurasa wake wa Instagram.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad