Harmonize Atangaza Kuacha Kuvuta Sigara Kisa Abby Chams

Harmonize Atangaza Kuacha Kuvuta Sigara Kisa Abby Chams

Harmonize Atangaza Kuacha Kuvuta Sigara Kisa Abby Chams

Harmonize ameonyesha mabadiliko makubwa kwenye maisha yake tangu alipoanza uhusiano na mpenzi wake mpya, @Abigail_Chams, ambaye amepewa jina la Furaha. Kupitia story yake ya leo kwenye Instagram, @Harmonize_tz amekiri kwamba amekubali kubadili tabia zake kwa ajili ya Furaha, hasa akizungumzia kuacha tabia ya kuvuta.


Akiandika, "Furaha hapendi harufu ya moshi wowote. Kwa hivyo sasa hivi nimeacha kuvuta rasmi," Harmonize alionyesha jinsi upendo kwa mpenzi wake umegusa maamuzi yake ya kimaisha. Aliendelea kusema kuwa, “Ni muda mwingi sasa, yeyote atayekuambia navuta kakuingiza chaka. Amani yake ndio jambo la msingi sana kwangu.”


Kupitia maneno haya, Harmonize alionyesha dhamira yake ya kuzingatia afya yake na amani ya Furaha na kumfanya ajivunie kwa kuwa tayari kubadili tabia ambazo alizozoea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad