“Baada ya kutekwa katika stendi ya Magufuli mashuhuda waliotoa taarifa ndio ambao walisaidia kwa sababu mashuhuda waliokuwa pale waliangalia vitu wakakuta ni vitu vya ACT (@actwazalendo_official ),hawana namba za viongozi wa ACT Wazalendo lakini mashuhuda kadhaa wana namba za aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kibamba John Mnyika. Na kwa sababu tukio lile lilitokea katika Jimbo la Kibamba,yeye akachukua taarifa hii kwa uzito, napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mnyika.
"Nichukue fursa hii kuwashukuru boda boda wote Tanzania wakiwakishwa na Bodaboda mwenzao aliyenisaidia pale Coco beach kwa sababu nilomba msaada kwa magari yaliyokuwa yanapita pale nikiyasimamisha nikiwa katikati ya barabara lakini hakuna magari yaliyosimama kwa sababu shati langu lilikuwa limechanika chanika suruali naishikilia labda hawakua na uaminifu na mimi, bodaboda mmoja nilipomsimamisha kumuomba msaada alienda kuchukua bodaboda wenzake na akaja kunisikiliza na wakaridhia kunisaidia"
"Nilipelekwa Aga Khan nikiwa hoi sana nawashukuru kwa huduma yao kwa kutoa huduma yao ya matibabu haraka na ya uhakika kuhakikisha figo yangu ambayo inakwenda kufeli inaimarika na kufanya kazi kwa sababu nilipofika pale walugundua kama figo inakwenda kufeli.
Polisi @polisi.tanzania hawapaswi kuchukua muda wowote wa kufanya uchunguzi dhidi ya tukio langu kwa sababu moja nimewapa ushirikiano wa kuchukua maelezo walikuja hospitali lakini mbili tukio langu ni rahisi ku-trace(kufuatilia hatua kwa hatua) walioniteka walisahau pingu katika kituo cha mabasi cha Magufuli na pingu hiyo ilikabidhiwa kituo cha polisi cha Magufuli Bus Stand na wlaihorodhesha kama moja ya vitu walivyoletewa na mashuhuda. Pingu zina serial number ni kama bunduki ambayo ina serial number kujua bunduki hii alipewa nani. Naamini kupitia ile pingu ni rahisi walioniteka kufahamika.”
“Lakini mbali na hapo mimi wakati natekwa simu yangu ilikuwa imezimika waliponifikisha huko waliponifikisha walininyang’anya simu wakaenda kuichaji wakaiwasha wakaja wakanifunua jicho moja na kunishikilia kichwa ili nisiwaone wakiniambia nitoe pattern (nywila) kwenye simu. Kwa hiyo ni rahisi polisi kufahamu simu yangu desemba 01, 2024 iliwashiwa wapi baada ya mimi kutekwa saa 10(Alfajiri).”
“Naomba niwaambie watanzania suala la ulinzi na usalama ni jambo ambalo tunapaswa tuungane kwa pamoja kupaza sauti zetu kupinga kukemea haya matendo. Na wala tusiseme kwamba haya matukio yanatokea kwa wakosoaji, viongozi wa vyama, wanaharakati kwamba wewe ambaye si mwanaharakati kwamba upo salama.”
“Kwamba wewe uko ndani ya chama cha mapinduzi unajiona uko salama tunajidanganya sana namna matukio haya yalipofikia sasa hivi sio ya vyama tena yameshavuka mpaka. Tarimo(mfanyabiashara Deogratius Tarimo) hajihusishi kabisa na siasa katekwa, umeona Dunstan hajihusishi kabisa na masuala ya kisiasa katekwa kwa hiyo tunapoendelea kukaa kimya tunazidi kuyalea haya matukio yaendelee kutokea.”
“kumekuwa na mwanya wa dhihaka na propaganda kwamba matukio haya ya utekaji sio ya ukweli ni ya kutengeneza ntu anawezaje kutengeneza kujiumiza, mtu anawezaje kutengeneza kujiumiza mguu manusura kufa”
“Nilimsikiliza hata Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa @gersonmsigwa akisema asilimia 80% ya matukio y utekaji ni ya kutengeneza kwamba asilimia 20% ndiyo ya kweli lakini nimezungumza hapa matukio 8 ambayo hayana uchunguzi basi kama ni ya kutengeneza fanyeni chunguzi mtuambie aliyemteka Soka, aliyemteka Sativa, aliyemteka na kumuua Ali Kibao, aliyeniteka mimi tupeni majibu”
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo amesema kuwa waliotekeleza tukio la kumteka siku ya Desemba 01, 2024 katika kituo cha mabasi cha Magufuli Dar Es Salaam walimuonya kuwa asielezee tukio la kutekwa kwake badala yake aende nyumbani moja kwa moja.
"Muliro (Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam) alivyohojiwa na vyombo vya habari, yaani yeye suala la waliomteka Nondo siyo 'ishu', usalama wa Nondo ukoje kwake siyo 'ishu', suala ambalo kwake alitilia maanani ni mtu aliyetekwa anawezaje kupanda bodaboda, mtu aliyetekwa anawezaje kwenda Makao Makuu asiende polisi?"- Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo @ngome_ya_vijana_taifa Abdul Nondo akizungumza na wanahabari leo Januari 09, 2025