Aliyekuwa kocha wa Yanga Sc, Miguel Angel Gamondi yupo ukingoni kutangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Raja Casablanca ya Morocco akichukua mikoba ya Ricardo Sa Pinto aliyetupiwa virago wiki iliyopita.
Gamondi raia wa Argentina anatarajiwa kuwa kocha wa tatu kuinoa Raja AC kama kocha mkuu msimu huu baada ya Ricardo Sa Pinto na Rusmir Cviko.
Cviko alichukua mikoba ya Josef Zinnbauer aliyeinoa klabu hiyo akisaidiwa na Fadlu Davids wa Simba Sc kwa mafanikio msimu uliopita huku klabu hiyo ikimaliza ligi bila kupoteza mchezo wowote.