Mwamuzi kutoka nchini 🇲🇷Mauritania Patrice Milazar ndiye amepewa jukumu la kuiamua mechi ya mwisho ya hatua ya makundi kati ya 🇹🇿Yanga dhidi ya 🇩🇿MC Algers.
Mchezo huo utapigwa Jumamosi hii na ni muhimu kwa timu zote mbili kwani Yanga itakuwa ikihitaji ushindi ili ifuzu hatua ya robo fainali huku MC Algers ikihitaji sare pekee.