Jeshi la Polisi @tanpol mkoani Arusha linafanya uchunguzi pamoja na kuwatafuta watu wote waliohusika katika tukio la wizi ndani ya gari aina ya Toyota Alphard lenye namba za usajili T. 340 EJR kama ilivyoonekana katika picha mjongeo (video) iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Januari 14.2025 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo amebainisha kuwa tukio hilo limetokea Januari 12 mwaka huu (2025) maeneo ya Kaloleni jijini Arusha ambapo mtu aitwaye Goodluck Matingisa (41) anadai kuibiwa mali zake
Kamanda Masejo amesema bado wanaendelea na uchunguzi kuhusina na tukio hilo na taarifa zaidi zitatolewa, aidha ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kubeba vitu vya thamani ndani ya magari yao bila kuwa na ulinzi na kuyaacha maeneo ya maegesho bila ya uangalizi wowote
Sambamba na hilo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika.