Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, SACP Muliro Jumanne Muliro amethibitisha jeshi la polisi kumshikilia Dkt. Wilbroad Silaa baada ya kumkamata usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2024.
Akizungumza kwenye kipindi cha Good morning cha Wasafi FM Muliro amesema “Daktari yupo tuko nae na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu na yeye yanakwenda vizuri”
Kamanda Muliro ameongeza kuwa wakati mahojiano yanaendelea wanaangalia taratibu za kisheria zinawaelekeza kufanya nini huku taarifa zaidi kutolewa baadae ”kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuambia nini cha kufanya na taarifa zaidi zitatolewa baadae” amesema Muliro
Ikumbukwe usiku wa kuamkia leo zimeenea taarifa kupitia mitandao ya kijamii zikidai Dkt. Silaa kukamatwa na watu aliodai kuwa ni polisi na wanampeleka kituo cha p
Polisi Mbweni.