John Heche: Kumuita Tundu Lissu Mropokaji ni Kosa....


John Heche: Kumuita Tundu Lissu Mropokaji ni Kosa....

 “Nawaomba wale Vijana wanaotembea wanatukana Viongozi waache, wengine wanajiita Viongozi wa Chama waache kutukana Viongozi, nani hajui gharama ambayo Tundu Lissu amelipa kwenye Chama hiki?, tunakuwa na Taasisi gani ambayo leo Mtu anayekemea rushwa anaitwa Mropokaji, kwamba tufiche madudu ndani ya uchafu? rushwa ni rushwa haina jina jingine, rushwa ni rushwa na tutaikemea, utofauti wetu na CCM Chama chetu kilijijenga katika kupigania Watanzania kuwa na Nchi ambayo haina rushwa”

“CHADEMA ilijengwa kwa kushambulia Mafisadi, Chama Kikuu cha Upinzani kilikuwa CUF kilipoona aibu kukemea rushwa kikafa Watanzania wakakihama, leo nani anasimama anasema tuogope kusema rushwa, ukila rushwa ndani ya Chama tutasimama na tutakutaja wewe ni mla rushwa, ukila rushwa ndani ya Serikali tutakutaja, tukiongoza Nchi ukala rushwa tutakufunga hata kama wewe ni Mwenzetu”

“Lissu ni Mkweli, ni Muadilifu, ni Muwazi, tunaweza kutofautiana mimi na yeye vitu vidogovidogo tu... wakati wa kusema............. hivyo ni vitu vya kawaida lakini Lissu ni Mkweli, Muadilifu, Muwazi na ni Msafi, na huyo ndiye atastahili kuwa Mwenyekiti wa Chama chetu kwa sasa, sijasikia Mtu anamtukana Mbowe kwa matusi lakini nimesikia Watu wanamtukana Lissu kwamba ni Mropokaji, hizi ni kauli za CCM lakini Wana CHADEMA?, rekodi za Lissu Bungeni? Lissu amekuwa Msema kweli siku zote, na huyo ndiye Mtu tunayemuhitaji” — Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa na Mbunge wa zamani wa Tarime Vijijini (2015 - 2020).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad