John Heche "Namuunga Mkono TUNDU Lissu Nagombea Umakamu"

 

John Heche "Namuunga Mkono TUNDU Lissu Nagombea Umakamu"

“Nimekaa kimya muda mrefu, nimetafakari muda mrefu, kwanini Watu wanaiunga mkono CHADEMA? kwanini leo kuna Watu wamepoteza maisha kwa ajili ya CHADEMA?, kila nikitoka nyumbani kwangu nje kuna kaburi la Mdogo wangu anaitwa Suguta aliuawa kwenye mapambano ya Chama hiki, sisi tuna alama ipo nyumbani pale, Watu wanatuunga mkono sio kwasababu ya rangi ya nguo tunazovaa ni kwasababu wanaamini tupo kwenye Taifa lililojaliwa rasilimali nyingi sana lakini Watu wetu ni masikini sana”


“Tuna rasilimali za kutosha, ardhi kubwa, mvua za kutosha lakini Watu wetu wanakufa Hospitali kwa magonjwa, Vijana wetu wanamaliza Vyuo hawana matumaini wanafanya betting na wengine wanajigeuza kuwa vibaka, hatuna chakula cha kutosha mpaka leo tunaagiza nje ya Nchi chakula kwasababu walio madarakani kwa miaka 60 wameshindwa kugeuza neema aliyotupa Mungu iwe baraka kwa ajili ya Nchi yetu”


“Haya mambo ndio waliyaona Waasisi wa Chama chetu wakasema tutaunda Chama ambacho kitaleta Viongozi Waadilifu na wenye msimamo ambao watapigania Mamlaka ya Nchi, wakipata Mamlaka ya Nchi wasigeuze kuwa mali yao bali wapiganie maslahi ya Wananchi”


“Leo tuna Watu wachache CHADEMA ambao wamepotoka ambao wanashindwa kujua dhima ya kuanzisha Chama hiki ni nini?, wanataka kufanya malengo ya Chama chetu kuwa malengo binafsi, sisi tunasema hatutokubali, hiki ni Chama cha Watanzania sio cha Wana CHADEMA ndio maana tunachangiwa na Watanzania wote kuendesha Chama hiki”


“Ninamuheshimu Freeman Mbowe na nampenda na nataka niseme mbele yenu kuwa Mbowe kwangu ni Baba wa siasa ambaye amenijenga na siwezi kusema jambo baya kuhusu Mbowe kuna mengi nasikia Watu wanazungumza lakini siwezi kusema, siwezi kutoka hadharani na kusema vibaya kuhusu Mbowe na leo nasema Mwenyekiti Mbowe kwa heshima tutakwenda kwenye Uchaguzi, tutakushinda, nitamuunga mkono Lissu na ninamuunga mkono na nimeamua kuchukua fomu baada ya Wananchi wengi kuongea na mimi kugombea Umakamu Mwenyekiti”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad