Meneja wa habari na mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amevunja ukimya wake baada ya mechi ya leo dhidi ya MC Alger. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, mechi ya Young Africans dhidi ya MC Alger ilienda sare ya sufuli. Yanga waliweza kupata pointi moja kwenye michuano hiyo na kufikisha pointi nane. Wapinzani wao waliweza kufuzu robo fainali baada ya Kufikisha pointi tisa kwenye msimamo wa kundi lao.
Kabla ya michuano ya leo, Young Africans ilikuwa na pointi saba na ilihitaji ushindi ili kufikisha pointi kumi ambazo zingewafanya kuungana na Al Hilal ya Sudan kwenda robo fainali. Al Hilal ya Sudan iliongoza kundi lao hata baada kupata kichapo kikali kutoka kwa TP Mazembe siku ya Jumamosi, Januari 18.
Ali Kamwe, Meneja wa habari na mawasiliano klabu ya Yanga ameshukuru wachezaji wake kwa kucheza vizuri licha ya kutopata ushindi. Ameeleza kuwa watajipanga wakati mwingine. Jambo ambalo limezua mijadala mbalimbali mitandaoni.