Kesi ya mauaji ya mtoto Grayson hadi Januari 27

"Mheshimiwa Hakimu, shauri hili liko mbele yako kwa ajili ya kutajwa na kwa sababu upelelezi bado unaendelea na hakimu anayesikiliza shauri hili hayupo, tunaomba kupangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amesema Patricia.

Baada ya ombi hilo, Hakimu Eligy pamoja na wakili anayemwakilisha mshtakiwa wa pili, Msangi, Luciana Nyondo, waliridhia ombi hilo na kesi kuahirishwa hadi Januari 27, mwaka huu.

Kelvin na Tumaini wanashtakiwa kwa kosa la mauaji ya mtoto Grayson Kanyenye (6) yaliyotokea Desemba 25, 2024, nyumbani kwa Hamis Mpeta, eneo la Ilazo Extension, aliyekuwa na uhusiano na mama mzazi wa mtoto huyo, Zainabu Shaban (Jojo).

 Jojo ambaye ni mfanyabiashara, wakati anaondoka alimwacha mtoto huyo mikononi mwa dereva bodaboda Joshua, baada ya kurudi asubuhi kutoka matembezini, alikuta ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kujeruhiwa maeneo ya shingoni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad