Aliyekuwa kocha wa Yanga raia wa Argentina 🇦🇷 Miguel Gamondi amekubali kujiunga na timu ya Al Nasr ya Libya 🇱🇾 baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili, tangu alipoachana rasmi na kikosi hicho cha Jangwani, Novemba 15, mwaka jana.
Taarifa kutoka Libya zinaeleza kocha huyo aliyeipa Yanga mafanikio zaidi amesaini mkataba wa miezi sita hadi mwishoni mwa msimu huu, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja, ikiwa kikosi hicho kitafanya vizuri kwenye michezo yao.