Kuhusu Dili la Bilioni 3.5 Kwa Mzize na Aziz K Kutua Wydad, Yanga Watoa Majibu Haya

 

Kuhusu Dili la Bilioni 3.5 Kwa Mzize na Aziz K Kutua Wydad, Yanga Watoa Majibu Haya

KLABU ya Wydad Athletic ya nchini Morocco imeendelea kuwasilisha maombi ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, lakini sasa imeongeza ikisema pia inahitaji huduma ya Stephanie Aziz Ki, imeelezwa.

Katika taarifa iliyotolewa na Wydad inasema wako tayari kulipa ada ya Dola za Marekani 800,000 kwa kila mchezaji sawa na jumla ya Dola Mil 1.6  sawa na zaidi ya Bilioni 3.5 ili wajiunge na timu yao inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Hata hivyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imewajibu Waarabu hao kuwa wachezaji hao hawauzwi kwa sababu ya ushiriki wa timu yao kwenye mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanayoshiriki.

“Hatuko tayari kuwauza wachezaji hawa kwa sababu ya ushiriki wetu katika mashindano ya CAF ya Ligi ya Mabingwa na tuna nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kocha Mkuu wa Wydad, Rulani Mokwena, ameieleza Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo kuwa anawahitaji wachezaji hao ili kuongeza nguvu katika kikosi chake.

Mokwena alianza kuvutiwa na wachezaji hao tangu akiwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ilipokutana na Yanga katika michuano hiyo ya CAF.

Yanga, wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itashuka dimbani huko Mauritania keshokutwa kuwakabili wenyeji Al Hilal na endapo itashinda mechi hiyo itajiimarisha kwenye mbio ya kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Al Hilal yenye pointi 10 na vinara wa Kundi A wameshafuzu hatua ya robo fainali na Yanga yenye pointi nne inahitaji ushindi tu ili kuendelea na kampeni yao katika michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad