Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mbowe apumzike kugombea nafasi ya uenyekiti na amuachie Makamu wa CHADEMA Bara Tundu Lissu awe Mwenyekiti wa Chama hicho.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo January 14,2025 amesema “Mwenyekiti Mbowe amekuwa kwenye Chama kwa miaka 30 na amekuwa Kiongozi wetu kwa miaka 21, Mwenyekiti ni Ndugu yangu, ni Kaka yangu tunatoka wote Machame lakini leo hapa nimekuja kutangaza kwamba katika uchaguzi huu unaofanyika keshokutwa nafanya uamuzi mgumu sana Mbowe ni Kaka yangu lakini leo nimekuja kumuomba apumzike amuachie Lissu afanye kazi ya uenyekiti, Mbowe apumzike apumzike”
“Na tunaposema apumzike hatumaanishi hana nguvu, inawezekana uwezo wake wa kuongoza umefika mwisho bila yeye kujua, kuna wakati kwenye hizi kazi unaona mivuragano hata Mimi niliiona pale Arusha hata kama mingine inachangiwa na Watu wa nje lakini niliona nikasema nikilazimisha kugombea ili nishinde itabidi nifungie Watu kwenye maghala, nikatangaza sitogombea uenyekiti wa Kanda”
“Ukaja uchaguzi wa Kanda niliona pia minyukano sikugombea, sasa nimekuja kumwambia Mwenyekiti haya majibizano mitandaoni na minyukano, nafahamu Katiba inamruhusu kuendelea lakini kwa sasa Watu wamepatikana wanataka nafasi yake na huwezi kumtilia mashaka Lissu ambaye amekuwa Makamu Mwenyekiti, Mnadhimu Mkuu wa Chama, Mwanasheria Mkuu wa Chama n.k, usipomuamini Makamu wako kumuachia Chama unataka kumuachia nani?”