Kumekucha Kariakoo, Biashara Kufanyika Masaa 24



DAR ES SALAAM; MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema mpango wa kufanya biashara kwa saa 24 kwenye eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, upo mbioni kuanza akisema kinachosubiriwa ni taarifa ya kutathimini mgawanyo wa wafanyabiashara wa usiku na mchana.

Amesema tathimini hiyo inayofanywa na timu ndogo iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, itaainisha namna ya kupunguza msongamano wa wafanyabiashara katika soko hilo mchana ili wengine wafanye biashara usiku.

Mpogolo alisema hayo juzi alipo zungumza na HabariLEO kuhusu hali na mwenendo wa wafanyabi ashara katika soko hilo la kimataifa.

Alisema serikali imeamua ku fanyia majaribio mpango huo katika Soko la Machinga Complex kufanya biashara kwa saa 24 na kugundua changamoto kadhaa ambazo sasa zinafanyiwa kazi katika Soko la Kariakoo kabla ya kuanza mpango husika.

Alibainisha kuwa kulingana na maandalizi yanavyokwenda, serikali inatarajia kuanza mpango huo mwis honi mwa mwezi huu au mwanzoni mwa Februari 2025.

Aliongeza kuwa utekelezaji wa mpango huo unafanyika kwa umaki ni mkubwa kwa kushirikisha wadau wote wanaohusika kama vile wadau wa usafiri na usafirishaji pamoja na wamiliki wa majengo katika maeneo ya biashara.

“Tunaendelea na ufungaji wa taa katika maeneo yote yatakayotu mika usiku kwa ajili ya biashara na tumewaomba wenye nyumba wote zinazozunguka eneo hilo wafunge taa na kamera ili kuzidisha usalama katika maeneo yao,” alisema.

Alifafanua kuwa serikali inaende lea kufanyia kazi miundombinu mbalimbali inayotakiwa katika ku fanikisha mpango huo wa kufanya biashara kwa saa 24.


Alisema ufungaji wa taa hizo pamoja na kamera utasaidia kuweka mazingira wezeshi kwa wafanya biashara kufanya shughuli zao bila kikwazo muda huo wa usiku. Katika hatua nyingine, Mpogolo alisema serikali kwa kushirikiana na viongozi wa wafanyabiashara wadogo imekutana na wadau mbalimbali kujadili na kuona njia nzuri ya utekelezaji wa mpango wa kuwapanga wamachinga ili kuon doka maeneo ya barabarani.

“Tumejitahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali wanaohusika moja kwa moja na shughuli za Kariakoo kama Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wamiliki wa hoteli, Jeshi la Polisi, wasafirishaji wa mizigo na kampuni za kubeba mizigo ili kupata utaratibu mzuri wa utekelezaji wa mpango huo,” alisema Mpogolo.

Aidha, Mpogolo alibainisha kuwa baada ya vikao kadhaa na wadau hao walikubaliana barabara na mitaa ambayo inatakiwa kuwa wazi bila kuwepo machinga kuwa ni Barabara ya Uhuru, barabara zote za mabasi yaendayo haraka na mitaa yote yenye benki.


Alisema halmashauri inaendelea kuhabarisha umma kuhusu utaratibu huo kwa kutumia magari mbalimbali yenye spika kubwa ili kila mfanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufahamu baadhi ya maeneo ambayo yanat akiwa kuachwa wazi ili shughuli za kijamii ziweze kuendelea.

Mpogolo alieleza kuwa mitaa mingi ya katikati ya Kariakoo itaendelea na shughuli zake kama kawaida ikiwemo mitaa maarufu hususani Congo, Nyamwezi na Sikukuu.


Aliwataka wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na serikali ili kufanikisha malengo mazuri ya seri kali ya kuwatengenezea mazingira bora ya kufanya biashara. Kuhusu usalama wa wananchi kwenda na kutoka sokoni waki fika katika maeneo yao usiku wa manane, Mpogolo alisema Jeshi la Polisi limeimarisha usalama hadi katika ngazi ya kata kwa kuimarisha ulinzi shirikishi, hivyo usalama wa watu na mali zao ni mkubwa.

Alibainisha kuwa kuanzishwa kwa biashara kwa saa 24 katika soko hilo kutakuja na fursa lukuki ikiwa ni pamoja na vijana wa usafirishaji kwa njia ya bodaboda na bajaji am bazo zitamhakikishia mwananchi kufikisha bidhaa zake nyumbani bila matatizo


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad