Kutokana na Nidhamu ya Mbosso, WCB Kumuachia Bila Kulipa Gharama Yoyote



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na @OfficialBabaLevo kupitia ukurasa wake wa Instagram, imebainika kuwa msanii @Mbosso_ amepewa uhuru wa kuondoka @WCB_Wasafi bila kulipa gharama yoyote.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na heshima kubwa ambayo Mbosso ameonyesha kwa @DiamondPlatnumz na viongozi wa WCB. Diamond ameamua kumsamehe malipo yote yanayohusiana na kuondoka kwake, hivyo kumpa nafasi ya kujitafutia mafanikio mapya kama msanii huru.

Baba Levo alidokeza kuwa WCB inapanga kusaini wasanii wapya tisa mwaka huu 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad