Kuwa na Fisi Kama Chombo Cha Usafiri, Mganga Matatani Simiyu

Kuwa na Fisi Kama Chombo Cha Usafiri, Mganga Matatani Simiyu


Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemkamata mganga wa kienyeji Emmanuel John Maduhu (31) kutoka kabila la Wasukuma akiwa na fisi hai. Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 24 Januari 2025, majira ya saa 12 jioni, katika kijiji cha Kilulu, Kata ya Bunamala, Wilaya ya Bariadi.


Kwa mujibu wa taarifa ya siku ya Jumamosi Januari 25, 2025 kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Edith Swebe, mganga huyo alidai kutumia fisi huyo katika shughuli za uganga wa jadi na pia kama "chombo cha usafiri anapopata kupaa angani."


Tukio hilo lilifanikiwa kutokana na jitihada za kikosi kazi cha Jeshi la Polisi kushirikiana na Mamlaka za Wanyamapori, ambapo baada ya uchunguzi wa awali kukamilika, mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ametoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kufuga fisi kwa kuwa wanyama hao ni hatari kwa maisha ya watoto na watu wengine. “Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la watoto kuliwa na fisi,” ameongeza.


Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa dhidi ya watu au vikundi vinavyohusiana na uhalifu wa kutumia kinga au vifaa haramu katika shughuli za tiba asili. Kamanda huyo amesisitiza umuhimu wa waganga wa tiba asili kufuata sheria, taratibu, na leseni katika utekelezaji wa shughuli zao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad