Lema Ashangazwa na CHADEMA Kutumia Walinzi Binafsi Kwenye Vikao Badala ya Wana Chama

Lema Ashangazwa na CHADEMA Kutumia Walinzi Binafsi Kwenye Vikao Badala ya Wana Chama


Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@chadematzofficial), @godbless_lema , amehoji vikali uamuzi wa chama hicho kutumia walinzi binafsi kulinda vikao vyao badala ya kutumia vijana wa hamasa na walinzi wa chama.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Lema ameonesha kushangazwa na mwelekeo wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wake unaotarajiwa kufanyika kesho, Jumanne, Januari 21, 2025.

"Unazuia impression ya wanachama wako kuja katika maeneo ya uchaguzi mkuu ndani ya chama? Hadi unaweka walinzi binafsi? Tumeanza lini hii tabia ya kukataa wanachama wetu kwenye mazingira ya vikao vyetu?" aliandika Lema kwa mshangao.

Aidha, Lema amewataka wajumbe wa chama hicho kutafakari kwa kina kabla ya kufanya maamuzi, akisisitiza kuwa viongozi Tundu @tunduantiphaslissu na @hechejohn ndio watu sahihi wa kukivusha chama kutoka katika changamoto zilizopo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad