Lissu "Mbowe Alidanganya Hakutaka Mimi Nigombee"




Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe amesema uongo kuwa waliwahi kujadiliana na Lissu akataka vyote Urais na Uenyekiti ambapo amesema sio kweli bali yeye alikuwa tayari kugombea Uenyekiti na amuachie Mbowe agombee Urais lakini Mbowe akakataa.

Akiongea leo January 06,2025 baada ya kuwasili Mwil. Nyerere Airport Jijini Dar es Salaam akitokea nje ya Nchi, Lissu amesema “Sio jambo zuri kusema Mwenyekiti amesema uongo, kwenye hili amesema uongo, tulikutana kwa siku 3 hapa Msimbazi Kanisani tukipatanishwa, tukizungumza juu ya hiki kinyang’anyiro, na kwa siku 3 zote Mwenyekiti alisema yeye hajaamua yeye hajaamua kugombea nafasi yoyote, Katibu Mkuu John Mnyika ni Shahidi”

“Nisiseme wengine waliokuwepo lakini Katibu Mkuu Mnyika ni Shahidi kwa siku 3 tukizungumza kwa pamoja, Mwenyekiti hataki Mimi nitie nia lakini akiulizwa wewe anasema ‘Mimi sijaamua’ kwa siku 3, sijawahi kuzungumza nae chochote nje ya hapo, kwenye hizo siku 3 Mimi nikasema tunakoenda sio kuzuri Mimi nipo tayari nigombee Uenyekiti wa Chama Urais nimuachie Mwenyekiti akakataa katakata”

“Kwahiyo habari kwamba Mimi nataka vyote siridhiki, Mwenyekiti amedanganya, alikataa Mimi nisigombee Uenyekiti wala Urais akasema inabidi tuangalie kwanza tupime upepo sijui nini ila yeye akasema hajaamua”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad